COVID-19 Ni Nini?

Ugonjwa wa COVID-19 ni ugonjwa ulio anza kuitwa Coronavirus. Coronavirus au COVID-19 ni ugonjwa unaoambukiza. Ugonjwa huu wa Coronavirus unasababishwa na virusi vipya ambovyo havijawahi kutambuliwa kwa wanadamu.

COVID-19 husababisha ugonjwa wa kupumua, homa na dalili kama ya kikohozi. Katika hali mbaya zaidi, ugonjwa huu husababisha ugonjwa wa Pneumonia au shida ya kupumua.

Pneumonia au shida ya kupumua ni ugonjwa ambayo huvimbisha pafu moja au mapafu zote mbili. Wakati coronavirus inakua pneumonia, sehemu za hewa zinaweza kujaa na maji. Ugonjwa huo wa Pneumonia unaweza   kuwa hatari kwa mtu yeyote, lakini haswa kwa watoto wachanga, watoto wa umri yeyote na watu zaidi ya miaka 65 (au makumi sita natano)

Watu wazee, na watu walio na hali zingine za matibabu (kama vile Pumu (au Asthma), ugonjwa wa kisukari (au Diabetes), au ugonjwa wa moyo (au Heart disease), wanaweza kuwa katika hatari zaidi ya kuwa wagonjwa sana.

Unaweza kujikinga na Coronavirus kwa kunawa mikono yako mara kwa mara na epuka kugusa uso wako.

Dalili

Ugonjwa wa Coronavirus (au COVID-19) unaonekana na dalili kali kama vile

 • kutokwa na makamasi ya maji puani,
 • kikohozi
 • Homa
 • Kidonda cha koo
 • Ugumu wa kupumua

Kinga na Tiba

Hivi sasa hakuna tiba wala hakuna chanjo ya kuzuia ugonjwa huu wa coronavirus (au COVID-19). Hakuna dawa maalum ya kuzuia au kutibu ugonjwa huu wa coronavirus (au COVID-19).

Unaweza kupunguza hatari yako ya kuambukizwa kwa ku:

 • Osha mikono yako mara kwa mara
 • Funika pua na mdomo wakati wa kukohoa na kupiga chafya
 • Epuka mawasiliano ya karibu; uwe mita 1 na mtu yeyote aliye na dalili ya homa au mafua.

 

Jinsi Inavyo Sambaa

Coronavirus (au COVID-19) ina enezwa hasa kupitia kuwasiliana na mtu aliyeambukizwa na huo ugonjwa. Ugonjwa huu una sambazwa wakati wa kukohoa au kupiga chafya, au kugusa makamasi au mate ya mtu aliye ambukizwa.

Kujitunza

Ukijihisi wewe ni mgojwa au ikiwa una dalili dhaifu, kaa nyumbani hadi utakapo pona. Unaweza kupunguza dalili zako uki:

 • Pumzika na kulala
 • Weka joto chumbani
 • Kunywa maji mengi
 • Oga maji moto kusaidia kupunguza baridi kwenye koo

Vyanzo:

 • Idara ya Afya ya Australia
 • Shirika la Afya Duniani (WHO)

 

Kwa maelezo na habari zaidi za leo wasiliana na mamlaka ya afya katika nchi yako ya sasa

SUBSCRIBE TO AFYA YOUTUBE CHANNEL